Kesi ya Najib yaahirishwa

0
253

Mahakama nchini Malaysia imeahirisha kesi ya ubadhilifu wa mali ya umma inayomkabili aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Najib Razak.

Razak anakabiliwa na mashtaka matano ya kutumia vibaya madaraka yake pamoja na matumizi mabaya ya fedha za serikali zenye thamani ya Dola Milioni 150 za Kimarekani.

Mwanasiasa huyo amekanusha kuhusika na tuhuma hizo, ingawa tayari alikuwa akikabiliwa na mashtaka mengine Ishirini na Matano.