Kenya yaripoti mgonjwa wa kwanza wa corona

0
534

Kenya imetangaza kuwa na mgonjwa wa kwanza wa homa ya corona, ambaye ni mwanamke aliyeingia nchini humo akitokea nchini Marekani.

Waziri wa Afya wa Kenya, Mutahi Kagwe ndiye aliyetangaza kuwepo kwa mgonjwa huyo na kusema kuwa mwanamke huyo aliingia Kenya machi tano mwaka huu, lakini vipimo vya jana ndivyo vimeonyesha kuwa ana virusi hivyo vya corona.

Waziri Kagwe amesema kuwa, hali ya mgonjwa huyo inaendelea vizuri,  lakini ataendelea kuwa katika uangalizi maalumu hadi hapo itakapothibitika amepona kabisa homa hiyo ya corona.

Mwanamke huyo aliingia nchini Kenya kutoka Marekani kupitia London nchini Uingereza.