Kenya yaendelea na kampeni za lala salama

0
183

Wananchi wa Kenya wanaendelea kwenda katika vituo vyao vya kupigia kura, ili kuhakiki taarifa zao ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 9 mwezi huu.

Wakati wananchi hao wakiendelea kwenda katika vituo hivyo, Tume ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC) imethibitisha kuwa zaidi ya wananchi milioni 22 nchini humo wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi huo.

Katika kuhakikisha masuala ya amani na usalama wakati wa kupiga kura, waziri wa Usalama wa Ndani wa Kenya Dkt. Fred Matiang’i amewahakikishia wananchi nchini humo kuwa hali ya amani na usalama imeimarishwa hivyo wasiwe na hofu wakati wa kupiga kura.

Katika hatua nyingine wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi huo mkuu wa Kenya wanaendelea na kampeni zao huku wakiweka msisitizo wa kutekeleza ahadi zao kwa wananchi.

Ikiwa zimebaki siku tatu kuelekea uchaguzi huo, mgombea Urais kupitia Kenya Kwanza William Ruto na Raila Odinga kupitia Azimio la Umoja wanachuana vikali.