Kenya wafanya ibada maalum

0
283

Rais William Ruto wa Kenya amewataka raia wa nchi hiyo kuiombea nchi yao, ili Mwenyezi Mungu aweze kuleta neema.

Rais Ruto amesema hayo wakati wa Ibada maalum ya Kitaifa, iliyofanyika kwa lengo la kumuomba Mwenyezi Mungu kuondoa changamoto zinazolikabili Taifa hilo ikiwa ni pamoja na ukame na njaa.

Ibada hiyo imefanyika kwenye uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Kwa sasa Kenya inashuhudia ukame mkali zaidi kuwahi kutokea nchini humo, katika kipindi cha miaka 40.

Maafisa wa serikali ya Kenya wamesema kuwa takribani raia milioni 4.3 wa Taifa hilo wanahitaji msaada wa haraka wa chakula.