Kapembe azikwa Tanga

0
141

Mazishi ya mpiga picha na mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Joachim Kapembe, yamefanyika leo katika makaburi ya Kange mkoani Tanga.

Kabla ya mazishi hayo ndugu, jamaa na marafiki walipata fursa ya kuagwa mwili wa Kapembe wakiongozwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye.

Joachim Kapembe ambaye kituo chake cha kazi kilikuwa mkoani Manyara, alifariki dunia tarehe 13 mwezi huu baada ya kupata ajali ya baiskeli akishuka kutoka kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro.

Ameacha mke na watoto wawili.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake Lihimidiwe, Amen.