Mgombea wa upinzani katika uchaguzi mkuu uliofanyika Julai Saba mwaka huu nchini Cameroon, – Maurice Kamto amedai kuwa ameshinda.
Kamto ambaye ni kiongozi wa chama cha upinzani cha Rebirth of Cameroon (MRC) amejitangazia ushindi licha ya serikali ya nchi hiyo kumtaka asifanye hivyo.
Pamoja na kujitangazia ushindi, Kamto pia ametoa wito kwa rais Paul Biya ambaye ni mmoja wa viongozi wa Afrika waliokaa madarakani kwa muda mrefu kuachia madaraka kwa amani.
Hata hivyo mgombea huyo wa kiti cha urais nchini Cameroon kutoka upande wa upinzani hajatoa matokeo yoyote yanayomuonyesha kuwa yeye ni mshindi.
Mahakama ya katiba nchini Cameroon ndio chombo pekee nchini humo chenye mamlaka ya kutangaza matokeo rasmi ya uchaguzi mkuu ndani ya kipindi cha muda wa siku 15 tangu kufanyika kwa uchaguzi.