Kampuni kubwa ya maziwa yaomba radhi

0
170

Kampuni kubwa zaidi ya maziwa Korea Kusini imelazimika kuomba radhi, kufuatia tangazo lake ambalo limewaonesha Wanawake kama ng’ombe.

Video ya tangazo hilo imeonekana ikimuonesha mpiga picha wa kiume akiwarekodi kwa siri Wanawake wakiwa shambani, ambao baadaye wanabadilika na kuwa ng’ombe.

Baada ya kukosolewa na watu mbalimbali, kampuni hiyo imeondoa tangazo hilo kwenye mtandao wa YouTube, lakini kata hivyo limetazamwa na watu wengi zaidi baada ya watumiaji wa mtandao huo kulirudisha tena.

Watu wengine wamekosoa tabia iliyooneshwa katika tangazo hilo la kuwarekodi wanawake kwa siri, tabia ambayo imekuwa ikichukiwa na ni kinyume na sheria za Korea Kusini.