Joto la uchaguzi Ivory Coast lazidi kupanda

0
258
Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo

Mahakama ya katiba nchini Ivory Coast imemzuia Rais wa zamani wa nchi hiyo Laurent Gbagbo na aliyekuwa waziri mkuu, Guillaume Soro kugombea nafasi ya Rais katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao nchini humo.

Tume ya uchaguzi ya Ivory Coast tayari imetoa tamko kuwa mtu yeyote mwenye historia ya kesi ya jinai haruhusiwi kugombea nafasi ya urais.

Katika hatua nyingine, mapema waandamanaji wamejitokeza katika miji mbalimbali nchini humo kupinga mpango wa Rais Alassane Quattara kugombea nafasi ya urais kwa awamu ya tatu kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Quattara ameamua kutangaza kugombea baada ya aliyeterajiwa kuwa mrithi wake kufariki ghafa mwezi Julai mwaka huu.

Watu kumi na watano wamepoteza maisha katika vurugu zinazoendelea nchini humo tangu rais Quattara alipotangaza kuwa anagombea kwa awamu nyingine.