Jose Eduardo Dos Santos afariki dunia

0
162

Rais wa zamani wa Angola, Jose Eduardo Dos Santos amefariki dunia katika hospitali moja kwenye mji wa Barcelona nchini Hispania ambapo alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Kiongozi huyo ambaye amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79. amekuwa akipatiwa matibabu nchini Hispania tangu alipohamia nchini humo baada ya kuondoka madarakani nchini Angola mwaka 2017.

Jose Eduardo Dos Santos ameiongoza Angola chini ya chama tawala cha MPLA kwa kipindi cha miaka 40 tangu mwaka 1979 ambapo nchi yake ilikuwa mstari wa mbele katika mapamano ya ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika huku nchi yake ikikabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoendeshwa na aliyekuwa kiongozi wa kikundi cha waasi cha UNITA, Jonas Savimbi ambaye baadaye alikuja kuuawa.
 
Dos Santos alichukua madaraka nchini Angola baada ya kufariki kwa kiongozi aliyeongoza mapambano ya uhuru nchini humo Agostinho Neto.