Joe Biden aongoza katika kura za maoni

0
739

Aliyekuwa Makamu wa Rais nchini Marekani, Joe Biden ameendelea kuongoza katika kura za maoni za kumtafuta mgombea wa kiti cha urais nchini humo kupitia chama cha Democrat.

Licha ya kuwepo kwa virusi vya corona nchini Marekani vinavyosababisha shughuli nyingine kushindwa kuendelea kama zilivyopangwa, Biden amejipatia ushindi katika Jimbo la Florida na kumshinda mpinzani wake Bernie Sanders.

Biden pia ameendelea kuongoza katika majimbo ya Arizona na Illinois ambako alipata ushindi wa kishindo, licha ya Sanders kupata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa vijana.