Jeshi la Sudan kutoa taarifa kuhusu maandamano yanayoendelea

0
333

Habari kutoka nchini Sudan zinasema kuwa Jeshi la nchi hiyo muda wowote kuanzia hivi sasa linatarajiwa kutoa taarifa ya hali ilivyo sasa nchini humo kufuatia kuendelea kwa maandamano yanayoshinikiza kuondoka madarakani kwa Rais  Omar Al-Bashir.

Kwa mujibu wa habari hizo, kwa sasa mikutano mbalimbali inafanyika baina ya viongozi wa juu wa  Jeshi pamoja na  wa serikali ili kujadili nini cha kufanya kuhusu maandamano yanayoendelea.

Kwa siku kadhaa sasa, Raia wa Sudan wamekua wakiandamana katika mitaa mbalimbali ya mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum kushinikiza kuondoka madarakani kwa Rais Al-Bashir aliyeliongoza Taifa hilo  kwa muda wa miaka Thelathini.

Mamia ya waandamanaji hao pia walipiga kambi katika Makao Makuu ya Jeshi la nchi hiyo wakiwataka askari kuwaunga mkono katika kushinikiza kuondoka madarakani kwa Rais Al-Bashir.