Rais wa zamani Ufaransa, -Jacques Chirac amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 86.
Chirac amefariki Dunia hii leo akiwa na familia yake.
Chirac amekua Rais wa Ufaransa tangu mwaka 1995 hadi 2007 na pia amewahi kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo kwa vipindi viwili tofauti.
Akiwa Rais wa Ufaransa, ameliongoza Taifa hilo kuingia katika sarafu moja ya Ulaya.
Wakati wa kikao chao hii leo, Wabunge wa Bunge la Ufaransa wamesimama na kunyamaza kwa muda wa dakika moja, ili kuombomboleza kifo cha kiongozi huyo wa zamani wa nchi hiyo.