Watu wengine Saba kutoka katika Mamlaka ya Palestina wamekufa, baada ya vikosi vya Israel kurusha makombora kuelekea nchini humo na kufanya idadi ya watu waliokufa kutokana na mashambulio mbalimbali kufikia 17.
Wakati hayo yakiendelea, Misri yenyewe imeendelea kufanya usuluhishi kati ya nchi ya Israel, uongozi wa Wanamgambo wa Hamas kutoka Mamlaka ya Palestina pamoja na kikundi kimoja cha wapiganaji wa Kiislamu kutoka kwenye Mamlaka hiyo.
Misri inajaribu kufanya usuluhishi ili kuzuia mashambulio zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati, kwani Wanamgambo wa Hamas pia wamejibu mashambulio kwa kurusha makomboa ya roketi nchini Israel.
