Israel na Falme za Kiarabu zafikia makubaliano

0
311

Israel na Falme za Kiarabu (UAE) zimefikia makubaliano ambapo Israel imekubali kusitisha mipango yake ya kuchukua sehemu ya eneo la ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan.

Makubaliano hayo yanatarajiwa kuwa njia ya kupatikana kwa amani.

Habari zinasema Palestina imeshangazwa na hatua hiyo na Balozi wake katika Falme za Kiarabu amerejea nyumbani.

Kwa upande wake Rais wa Marekani Donald Trump amesema makubaliano hayo ni hatua muhimu na ya kihistoria.