Iraq waendelea kuandamana kuipinga Serikali

0
696

Polisi wa kutuliza ghasia nchini Iraq, wameendelea kupambana na Waandamanaji wanaoendelea na maandamano yao ya kuipinga Serikali katika mji mkuu wa nchi hiyo Baghdad na katika maeneo mengine.

Habari zinasema kuwa, watu kadhaa wamekufa na wengine kujeruhiwa katika mji wa Karbala katika maandamano hayo yanayohamasishwa na Wahitumu wa Vyuo Vikuu, wanaoishinikiza Serikali ya Iraq kuwapatia ajira, baada ya kuhitimu masomo yao na kukosa ajira.

Wahitimu hao wanadai kuwa, licha ya Serikali ya nchi yao kutoa ahadi mbalimbali, wanashindwa kuitumia elimu yao kujikimu na kwa maendeleo ya Taifa lao na hivyo kuwafanya kukata tamaa ya maisha.