IFAD yajadili maendeleo ya uvuvi wa Tanzania

0
350

Mkutano wa Mfuko wa Maendeleo wa Kilimo na Uvuvi Duniani (IFAD) umeanza leo ukihudhuriwa na Rais wa Mfuko huo, Alvaro Lario na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mahmoud Thabit Kombo ambaye pia ni mwakilishi wa kudumu wa mfuko huo akiiwakilisha Tanzania.

Miongoni mwa masuala muhimu yaliyojadiliwa katika mkutano huo ni miradi ya uvuvi kwa Tanzania Bara na Zanzibar ambayo inafadhiliwa  chini ya mkopo nafuu wa mfuko huo. 

Miradi hiyo ni pamoja na mradi wa ujenzi wa meli za uvuvi, ujenzi wa masoko, majokofu ya baridi ya kuhifadhi samaki na mazao ya baharini ikiwemo mwani.

Wengine waliohudhuria mkutano huo ni waziri na katibu wakuu wawili wa wizara ya Mifugo na Uvuvi kutoka Tanzania Bara na Uchumi wa Buluu na Uvuvi kutoka  Zanzibar pamoja na timu ya maafisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Italia wakiongozwa na Mwambata wa Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Misitu, Jaquiline Mhando.

Mkutano huo unatarajiwa kumalizika Februari 16, 2023.