Idadi ya watu waliokufa katika mashambulio ya kigaidi yaliyofanywa nchini Niger katika vijiji viwili imefikia 100, huku wengine wengi wakiwa wamejeruhiwa.
Serikali ya Niger inafanya uchunguzi kuwabaini watu waliohusika na mashambulio hayo ya kigaidi na kusisitiza kuwa sheria itachukua mkondo wake.
Mara kadhaa nchi ya Niger imejikuta ikikumbwa na mashambulio ya kigaidi ambayo yanadaiwa kufanywa na vikundi mbalimbali vya watu wenye silaha, wakiwemo Wanamgambo wa Boko Haram kutoka nchini Nigeria.
Eneo lililoshambuliwa nchini Niger linapakana na nchi za Mali, Burkina Faso na Benin.