Idadi ya vifo China yaongezeka

0
355

Idadi ya vifo vya  watu walioathirika na ugonjwa unaotokana na virusi vya corona nchini China imeongezeka na kufikia ishirini na sita.

Hadi sasa zaidi ya kesi 830 za waathirika wa ugonjwa huo zimeripotiwa huku tayari nchi hiyo imezuia watu kusafiri ndani na nje miji ya nchi hiyo.

Pia imepiga karantini mikusanyiko ya watu ikiwemo sherehe mbalimbali zinazofanyika kuelekea mwaka mpya wa nchi hiyo ikihofiwa kuenea zaidi kwa ugonjwa huo.

Tayari nchi za Singapore Thailand, Korea Kusini na Japan zimeripoti kusambaa kwa ugojwa huo nchini mwao.

Shirika la afya duniani WHO limesema ni mapema kutangaza ugonjwa huo kuwa ni janga la kimataifa lakini ni hatari na tishio nchini china.