ICC yatoa hati ya kukamatwa kwa Rais Putin

0
224

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetoa hati ya kukamatwa kwa Rais wa Urusi, Vladmir Putin na afisa wa Urusi, Maria Lvova-Belova kwa madai ya mpango wa kuwahamisha kwa nguvu watoto wa Ukraine kwenda Urusi.

Kwa mujibu wa ICC, Putin anabeba jukumu la jinai binafsi kwa kuwafukuza kwa lazima watoto wa Ukraine.

Mahakama imedai kuwa alitenda makosa hayo moja kwa moja au kwa ushirikiano na wengine, au alishindwa kuwazuia wasaidizi chini ya mamlaka yake.