Hofu dhidi ya chanjo ya UVIKO yazidi

0
293

Mamlaka za afya katika mataifa ya Denmark, Norway and Iceland pamoja na mataifa mengine ya ulaya, zimepiga marufuku chanjo ya covid-19 (UVIKO-19) ya AstraZeneca.

Wakati nchi hizo zikipiga marufuku chanjo hiyo, Serikali za Thailand na Bulgaria, nazo zimetaka kufanyika kwa uchunguzi wa kina kuhusu chanjo hiyo.

Hatua hiyo imefikiwa  baada ya baadhi ya waliopata chanjo hiyo kuanza kupata tatizo la kuganda kwa damu, huku vikiripotiwa vifo kadhaa miongoni mwa waliopatiwa chanjo hiyo.

Habari iliyoenea zaidi ni ile inayomuhusu mama mwenye umri wa  miaka 60,  ambaye alipatiwa chanjo hiyo na kuanza kupata tatizo la kuganda kwa damu.

Hali hiyo pia imeyafanya mataifa ya Austria na Italia kuzuia chanjo dhidi ya covid 19 hadi uchunguzi ufanyike, ambapo tayari watu wawili huko Sicily wamefariki dunia.

Bingwa wa chanjo Profesa Helen Petousis-Harris kutoka chuo kikuu cha Auckland amesema,  ni vema utafiti wa kina ukafanyika ili kubaini ukweli kuhusu chanjo hiyo ya AstraZeneca.

Mapema mwezi Februari, nchi ya Afrika Kusini nayo ilizuia matumizi ya chanjo ya AstraZeneca kwa kusema haikuwa na kinga ya kutosha dhidi ya virusi hivyo