Uongozi wa jimbo la California nchini Marekani umetangaza hali ya tahadhari baada ya moto wa msituni kuendelea kuteketeza misitu katika jimbo hilo na maelfu ya watu kulazimika kuyahama makazi yao.
Hali hiyo ya tahadhari imelazimika kutangazwa baada ya mioto kadhaa ya msituni kuanza kulipuka katika jimbo hilo la California bila utaratibu, huku ikichochewa na upepo mkali unaoambatana na ukame.
Zaidi ya watu Elfu Mbili wamelazimika kuyahama makazi yao na kwenda katika maeneo salama, huku moto huo ukiwa tayari umeteketeza maelfu ya hekari za misitu.