Hali si shwari CAR

0
218

Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) imetangaza hali ya tahadhari, wakati vikundi vya watu wenye silaha vikijaribu kuweka vizuizi vya kuingia katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui.
 
Amri hiyo inatarajiwa kudumu kwa muda wa siku 15.
 
Waasi wanadaiwa kushikilia sehemu kubwa ya nchi hiyo, huku wakitaka Rais Faustin Touadera aliyeshinda katika uchaguzi uliofanyika mwezi Desemba mwaka 2020 ajiuzulu.
 
Aidha Mahakama ya Katiba katika Jamhuri hiyo ya Afrika ya Kati imethibitisha ushindi wa Toudera katika uchaguzi huo.
 
Wiki iliyopita, Waasi walishambulia baadhi ya maeneo yaliyo nje ya mji wa Bangui.