Wabunge nchini Lebanon wamekutana kujadili suala la kuongeza muda wa hali ya tahadhari katika Mji wa Beirut kufuatia mlipuko uliotokea katika mji huo wiki iliyopita.
Polisi wameimarisha ulinzi katika eneo ambalo mkutano huo unafanyika ili kudhibiti waandamanaji.
Habari kutoka nchini Lebanon zinasema madhara na hasara iliyosababishwa na mlipuko huo inakadiriwa kufikia zaidi ya dola za kimarekani bilioni 15.