Guinea watakiwa kumaliza mgogoro wa kisiasa

0
777

Umoja wa Mataifa umetaka kufanyika kwa majadilinao ya Kitaifa nchini Guinea, ili kumaliza mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini humo.

Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kukamilisha ziara yake katika nchi jirani ya Liberia, Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika nchi za Afrika Magharibi, – Mohamed Ibn Chambas amesema kuwa hali iliyopo sasa nchini Guinea haipaswi kufumbiwa macho.

Chambas amesisitiza kuwa, Raia wote wa Guinea wanatakiwa kukaa katika meza ya majadiliano, ili kuondoa tofauti miongoni mwao na kuamua namna ya kufanya uchaguzi.

Kwa wiki kadhaa sasa Raia wa Guiunea wamekua wakiandamana, baada ya kupata fununu kuwa Rais Alpha Conde wa nchi hiyo ana mpango wa kubadili Katiba ili aweze kugombea kwa kipindi cha Tatu katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka 2020.

Rais Conde amekua Rais wa Guinea tangu mwaka 2010 na kipindi chake cha Pili kinamalizika mwaka 2020.