FAO yaelezea wasiwasi wake kuhusu nzige

0
402

Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu uwezekano wa kutokea njaa kwa nchi za Afrika Mashariki iwapo nzige waliovamia baadhi ya nchi katika eneo hilo hawatadhibitiwa.

Kufuatia hali hiyo, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kusaidia fedha pamoja na vifaa kwa ajili ya kudhibiti nzige hao ambao tayari wamevamia nchi za Ethiopia, Somalia, Kenya na Uganda.

Mkurugenzi wa kitengo cha kukabiliana na majanga cha FAO, -Dominique Burgeon amesema kuwa, jitihada za haraka zinahitajika kuwadhibiti nzige hao ambao endapo wataachwa na kuzaliana watasababisha janga la njaa.