Familia zaruhusiwa kuzaa watoto watatu

0
164

Serikali ya China imetangaza kuwaruhusu Wananchi wake kuongeza idadi ya watoto wanaopaswa kuzaliwa katika familia moja.

China imetangaza kuwa sasa familia moja inaruhusiwa kuzaa watoto watatu, badala ya wawili kama ilivyokuwa imetangaza mwaka 2016.

Kwa miaka mingi China ilikuwa ikisimamia zoezi la uzazi wa mpango na kuwazuia Wananchi wake kuzaa zaidi ya mtoto mmoja.

China ndilo Taifa linaloongoza duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya watu.