Ebola yadhibitiwa DRC

0
150

Maafisa wa afya wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wametangaza kudhibitiwa kwa wimbi la kumi na tatu la ugonjwa wa Ebola, ambapo watu 11 waliagua huku sita wakifariki dunia.

Maambukizi hayo yalitokea mwezi Oktoba mwaka huu katika eneo la Beni, kwenye jimbo la North Kivu Mashariki mwa Jamhuri hiyo.

Wimbi hilo lilizua hofu na taharuki kwa wananchi wa DRC, kufuatia wimbi la maambukizi ya Ebola lililotokea kati ya mwaka 2018 na 2021 kusababisha vifo vya takribani watu 2,300.