Dunia yamlilia Mtukudzi

0
1367

Watu mbalimbali wakiwemo wasanii wameendelea kutuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu na jamaa wa Mwanamuziki maarufu wa nchini Zimbabwe na Afrika, – Oliver Mtukudzi kufuatia kifo cha mwanamuziki huyo.

Baadhi ya wasanii hao ni wale wanaounda kundi la  Sauti Sol la nchini Kenya na Daniel Mhlanga.

Mtukudzi amefarika dunia Januari 23 mwaka huu  katika hospitali moja mjini Harare akiwa na umri wa miaka 66.

Habari zaidi kutoka mjini Harare zinasema kuwa  Mtukudzi amekuwa akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo kwa takribani mwezi mmoja.

Katika siku za hivi karibuni, msanii huyo alilazimika kufuata baadhi ya ziara zake za muziki katika nchi mbalimbali duniani,  kutokana na kuugua.

Muziki wa mwanamuziki huyo wa Zimbabwe, -Oliver Mtukudzi unafahamika kuwa ni wa miondoko ya Afro-Jazz na umevuka mipaka na kupata mashabiki wengi kote duniani.

Mtukudzi amekuwa katika taaluma ya muziki kwa zaidi ya miongo mine na kufanikiwa kutoa albamu 67.

Albamu ya mwisho ya  Mtukudzi imeangazia hali ya kisiasa  ilivyo hivi sasa nchini Zimbabwe na matatizo mengine ya kijamii.