Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stergomena Tax amewataka watanzania wote wanaoishi nje ya nchi kufuata sheria za Tanzania kwa kutojiunga na makundi ya kijeshi kwenye nchi wanamoishi.
Dkt. Tax ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari, kufuatia kifo cha Mtanzania Nemes Tarimo aliyefariki dunia katika vita inayoendelea kati ya Urusi na Ukraine.
Amesema Nemes alikuwa akipigana vita akiwa upande wa kikundi kimoja cha kijeshi cha Urusi akitokea jela alikokuwa anatumikia kifungo cha miaka saba baada ya kupatikana na makosa uhalifu.
Dkt. Tax amewaambia waandishi wa kuwa awali Nemes
alikuwa Urusi kwa ajili ya masomo ya chuo kikuu, lakini alikutwa na hatia ambapo alifungwa jela na baadaye kutolewa kwa makubaliano ya kulipwa fedha na kuachiwa huru baada ya kurudi kutoka vitani.
Amesema mwili wa Nemes umesafirishwa hii leo kutoka Urusi kuja Tanzania kwa ajili ya mazishi.