Dkt. Rioba ashiriki mkutano wa Afrika na SABA

0
422

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha akiwa na watendaji wengine wa vyombo vya habari vya umma na serikali, katika mkutano wa Utangazaji na vyombo vya Habari vya Kidigitali Afrika unaoendelea Kigali nchini Rwanda.

Mkutano huo unafanyika pamoja na mkutano wa mwaka wa vyombo vya habari vya Umma na Serikali Kusini mwa Afrika (SABA).

Miongoni mwa ajenda zinazojadiliwa katika mkutano huo ni vyombo vya habari vya Afrika kwenda na kasi ya mabadiliko ya utangazaji ya kidigitali, ili kutangaza maudhui ya kiafrika ipasavyo.