Corona yazuia Mahujaji kwenda Saudi Arabia

0
450

Saudi Arabia imesimamisha utoaji wa viza kwa mahujaji wanaotaka kwenda kuhiji kufuatia mlipuko wa virusi vya Corona ambavyo vimeendelea kuleta athari katika maeneo mbalimbali duniani.

Mahujaji waliokuwa wakitarajia kwenda kutekeleza moja kati ya nguzo za dini ya Kiislamu huko Saudi Arabia, kwa sasa wanalazimika kuahirisha safari zao.

Saudia Arabia imesisitiza kuwa, haitaweza kuwahudumia maelfu ya watu watakaoingia nchini humo na kuhakikisha kuwa hawaambukizwi virusi vya corona.