Corona yaua watu elfu nne ndani ya siku moja

0
273

Brazil imetangaza kuwa takribani watu elfu nne wamekufa katika kipindi cha siku moja baada ya kuugua corona, hali inayoifanya nchi hiyo kuongoza duniani kwa mara nyingine kwa vifo vinavyotokana na ugonjwa huo.

Licha ya Brazil kuongeza mapambano dhidi ya corona, vifo vimekuwa vikiongezeka kila siku huku maambukizi nayo yakiendelea kuwa juu.

Hivi sasa mazishi ya watu waliokufa kwa ugonjwa huo yanalazimika kufanyika hadi usiku, kwa kuwa idadi ya watu wanaohitaji huduma hiyo imeongezeka.

Habari zaidi kutoka nchini Brazil zinaeleza kuwa, hospitali zimeendelea kulemewa na wagonjwa, na kusababisha wagonjwa wengi kutopata huduma zinazostahili.

Vifo vya wagonjwa wa corona vinaendelea kuongezeka nchini Brazil katika kipindi hiki ambacho nchi hiyo imekuwa ikiendelea kuwapatia chanjo Wananchi wake dhidi virusi vya corona.