Corona yabisha hodi Rwanda

0
518

Wizara ya Afya ya Rwanda imetangaza nchi hiyo kuwa na mgonjwa wa kwanza wa homa ya corona.

Mgonjwa huyo raia wa India, alingiia nchini Rwanda Machi 8 mwaka huu.

Rwanda inakua nchi ya pili kwa nchi za Afrika Mashariki kutangaza kuwa na mgonjwa wa homa ya corona.

Hapo jana Kenya ilitangaza kuwa na mgonjwa wa Corona ambaye aliingia nchini humo akitokea Marekani, kupitia jijini London nchini Uingereza.