Corona: China kuwapima tena wakazi wote wa Wuhan

0
570

Serikali ya China imesema ina mpango wa kuwapima tena wakazi wote wa mji wa Wuhan kuona kama wameathiriwa na virusi vya Corona, baada ya kuonekana kwa maambukizi mapya katika mji huo ambao ulikuwa kitovu cha lipuko wa Corona.

Watu sita wamethibitika kuambukizwa Corona mjini Wuhan, yakiwa ni maambukizi mapya, tangu ugonjwa huo ulipolipuka kwenye mji huo na kisha kutokomezwa, na watu kuanza kurejea katika maisha yao ya kawaida.

Kumekuwa na kampeni mbalimbali mjini Wuhan zinazofanywa na wanaharati mbalimbali wanaosaidiana na serikali ya nchi hiyo, kuhamasisha watu kuwa tayari kupimwa tena kama wameambukizwa Corona.