Matokeo ya awali ya uchaguzi Mkuu uliomalizika hivi karibuni nchini nchini India yanaonyesha kuwa, chama cha BJP kinachoongozwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Narenda Modi kinaongoza.
Kufuatia matokeo hayo yanayompa matumaini ya kuliongoza taifa hilo la India kwa muhula mwingine, Waziri Mkuu Modi ametangaza kuendelea kujenga taifa lenye nguvu na umoja.
Baadhi ya Raia wa India wamesema kuwa, wamempa ridhaa Modi ya kuendelea kuliongoza taifa hilo ambalo ni la pili duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya watu, kwa vile wana matumaini kuwa ataweza kuwapatia ajira zaidi.
