Burundi imeiomba Tanzania kuendelea kuisemea katika majukwaa ya Kimataifa ili iondolewe vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya.
Ombi hilo limetolewa mkoani Kigoma na Katibu Mkuu wa wizara ya Mambo ya Nje wa Burundi Isdore Ntirampeba wakati wa ufunguzi wa mkutano wa sita wa Tume ya pamoja ya kudumu kati ya Tanzania na Burundi (JPC).
Ntirampeba amesema endapo Burundi itaondolea vikwazo hivyo ya kiuchumi itaendelea kupiga hatua kiuchumi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amesema lengo la mkutano huo wa sita wa Tume ya pamoja ya kudumu kati ya Tanzania na Burundi ni kuimarisha uhusino baina ya mataifa hayo mawili.