Buhari aahidi uchaguzi huru

0
1037

Rais Muhamadu Buhari  wa  Nigeria amesema kuwa  serikali yake itahakikisha uchaguzi mkuu unaofanyika hapo kesho  unakua huru na  wa haki.

Akilihutubia Taifa kupitia Televisheni  ya nchi hiyo, Buhari amesema kuwa  Nigeria ambalo ndilo Taifa imara zaidi kiuchumi Barani Afrika ni lazima lionyeshe mfano katika masuala ya kidemokrasi kwa kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika katika mazingira ya amani na utulivu.

Ametoa wito kwa  Raia wote wa nchi hiyo na hasa vijana kutotumiwa na Wanasiasa kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani wakati wote wa upigaji kura na wakati wa kusubiri matokeo.

Katika uchaguzi huo,  Rais Buhari anayewania muhula mwingine wa uongozi atapambana na kiongozi mkuu wa upinzani wa Nigeria, -Atiku Abubakar ambaye ni Mfanyabiashara tajiri na Makamu wa zamani wa Rais wa nchi hiyo.

 Zaidi ya  Raia Milioni 80  wa Nigeria wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi huo Mkuu.