Bruce Willis aachana na filamu

0
4753

Familia ya mcheza filamu wa Marekani Bruce Willis imetangaza kuwa mwigizaji huyo mwenye umri wa miaka 67 anastaafu kuigiza filamu za kulipwa baada ya kubainika kuwa na Aphasia, ambayo ni changamoto ya matamshi inayosababishwa na ubongo kuwa na tatizo linaloathiri uwezo wa mtu kuwasiliana.

“Kutoka na hili, baada ya kutafakari kwa muda Bruce ameamua kuacha na tasnia hii ambayo ina maana kubwa sana kwake,” imeeleza sehemu ya taarifa ya familia.

Maisha yake ya uigizaji yalianza mwanzoni mwa miaka ya 1970 akicheza nafasi ambazo hazikuwa rasmi katika filamu kama The Verdict. Nyota yake iling’aa na kuanza kutambulika zaidi na kujizolea umaarufu katika filamu ya Die Hard ya mwaka 2007 ambapo alitambulika zaidi kama John McClane na pia amefanya vizuri zaidi Katika filamu kadhaa ikiwemo Moonlight ya mwaka 1985, The roast of Bruce Willis ya mwaka 2018 kutokana ushiriki wake mkuu katika filamu hizo