Boris Johnson anusurika kung’olewa madarakani

0
250

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amenusurika kuondolewa madarakani kufuatia kura ya maoni ya kutokuwa na imani naye iliyopigwa na wabunge kutoka chama chake cha Conservative.

Katika kura hiyo iliyohusisha wabunge 359, kura 211 zimemuunga mkono huku 148 zikimkataa.

Wabunge wa chama cha Conservative wamepiga kura hiyo kufuatia kashfa inayomkabili kiongozi huyo pamoja na maafisa wa serikali ya kuvunja sheria ya UVIKO – 19 iliyokuwa ikizuia mikusanyiko ya watu.

Waziri Mkuu huyo wa Uingereza, Boris Johnson pamoja na maafisa hao
walihudhuria sherehe zilizohusisha upigwaji wa muziki na kunywa pombe katika mtaa wa Down jijini London.

Maafisa kadhaa wa Serikali ya Uingereza wamejiuzulu kufuatia kashfa hiyo huku taarifa kuhusu uchunguzi wa tukio hilo iliyotolewa hivi karibuni ikieleza namna viongozi hao walivyoshiriki katika sherehe hizo batili.