Bilionea wa Japan anatafuta mpenzi wa kwenda nae mwezini

0
368

Bilionea wa Kijapani Yusaku Maezawa anatafuta rafiki wa kike wa kuungana naye katika safari ya kuzunguka Mwezi.

Dada huyo atakuwa sehemu ya makala na mada ya mpango mpya wa filamu ya kumbukumbu, ili kuleta mjadala wa kuvutia wajasiriamali huko mbeleni.

Maezawa mwenye umri wa miaka 44 na rafiki huyo wa kike anatakiwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 20 ili kufanya onyesho hilo ambalo litaoneshwa AbemaTV.

“Kama hisia za upweke zinaanza kunizidi polepole, kuna jambo moja ambalo naendelea kuliwaza ni kuendelea kumpenda mwanamke mmoja,” ameandika Maezawa kuvutia waombaji.

Makala hiyo itaitwa “Full Moon Lovers”, pia itaoneshwa katika Tv za mitandao ya kijamii ili kulenga watazamaji ambao wameachana na TV za jadi.

Katika vigezo vya waombaji lazima awe binti mwenye hamu na nia ya kwenda kwenye safari za anga, aweze kushiriki katika utayarishaji wake na kuwa mtu anayetaka amani ya ulimwengu.