Bilionea Bill Gates na mkewe waachana

0
230

Mwanzilishi na mmiliki wa Microsoft, bilionea Bill Gates (65) na mkewe, Melinda Gates (56) wametangaza kutalikiana baada ya miaka 27 ya ndoa yao kwa maelezo kuwa wameona hawaweze kuendelea kuwa pamoja kama wanandoa.

“Baada ya kutafakari kwa kina na kufanya masuala mengi katika uhusiano wetu, tumefikia makubaliano kuvunja ndoa yetu,” umeeleza ujumbe wa wanandoa hao kupitia Twitter (Tafsiri ni ya mwandishi).

Wawili hao ambao kwa pamoja wana watoto watatu walikutana mwaka 1987 wakati Melinda alipojiunga Microsoft.

Licha ya kuvunjika kwa ndoa yao, matajiri hao wanatarajiwa kuendelea kushirikiana kwenye kazi zao za kuisaidia jamii kupitia Bill & Melinda Gates Foundation ambapo wamejikita katika masuala ya elimu, afya na usawa wa kijinsia.

Kwa mujibu wa Forbes, Bill Gates ni tajiri wa nne dunia akiwa na utajiri wenye thamani ya $124 bilioni, sawa na shilingi trilioni 287.6.