Sio jambo la ajabu kuona bia au mvinyo unatumika kama kifungua kinywa kwa jamii mbalimbali.
Nchini Ufaransa ifikapo saa tatu asubuhi ni utamaduni wao kupata kifungua kinywa cha mvinyo pamoja na vinywaji vingine.
Kwa nchi nyingine kama Uturuki ni kawaida kuona watu wakifungua kinywa kwa mkusanyiko wa vyakuwa vingi, meza zao hujazwa hadi sahani tisa zenye mkusanyiko wa vitafunwa vya aina mbalimbali.
Iliyotia fora zaidi ni ya jimbo la Bavaria nchini Ujerumani. Jimbo hilo linasifika kwa aina ya mavazi yake ya kiutamaduni na aina ya upishi wa vyakula vyao ambayo huakisi maisha yenye furaha wakati wote.
Jimbo hilo hupendelea kifungua kinywa cha pishi liitwalo “Weißwurstfrühstück”. Kifungua kinywa hicho cha kimila kinajumuisha Soseji na Bia na kinadhaniwa kuwa ndio mlo wa Kijerumani maarufu zaidi nchini humo.
Kusini mwa Munich, ipo baa moja ambayo yenyewe inakusanya umati wa watu kwa ajili ya kujipatia kifungua kinywa cha Bavaria-“Weißwurstfrühstück” ambacho ni kifungua kinywa cha Soseji nyeupe na pretzels laini ikiwa imeoshwa na kuandaliwa kwa kutumia bia.
Kwa mujibu wa Bodi ya Utalii ya Munich ‘Weißwurstfrühstück’ ni zaidi ya mlo na ni mlo maarufu zaidi nchini humo ambao kwa mara nyingi unatumiwa katika mikutano isiyo rasmi pale ambapo kahawa imechelewa.