Basi laua 25 na wengine kadhaa kujeruhiwa

0
431

Watu ishirini na tano wamekufa na wengine kumi na tatu kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wamepanda kusesereka katika bonde na kutumbikia katika mto nchini Indonesia.

Basi hilo lilibeba abiria thelathini na saba akiwemo dereva lililkuwa likitokea katika mji wa Bengkulu likielekea katika mji wa Palembang kusini mwa kisiwa cha Sumatra.

Zaidi ya waokoaji mia moja wamepelekwa katika eneo hilo kuwatoa majeruhi na miili ya watu waliokufa katika katika mto ambao basi hilo limetumbukia.