Baraza la Mawaziri kujadili mgogoro wa Uchumi nchini Lebanon

0
399

Baraza jipya la mawaziri lililoteuliwa nchini Lebanon linatarajiwa kukutana muda mchache ujao kujadiliana jinsi ya kuongoza taifa hilo hasa kukabiliana na mgogoro wa uchumi ambao umekuwa chanzo cha maandamano makubwa nchini humo.

Baraza hilo jipya la mawaziri limechaguliwa nchini Lebanon, baada ya mfululizo wa maandamano ya kupinga serikali na sera zake, ambazo waandamanaji wanasema zinaendelea kuwakandamiza na kufanya maisha yao kuendelea kuwa magumu.

Wananchi mara kadhaa waliandamana kupinga uteuzi wa mawaziri wakuu walioteuliwa na Rais Michelle Aoun wa nchi hiyo kwa madai kuwa wote wana uhusiano na utawala uliopo sasa hivyo hawawezi kujua shida za wananchi wa kawaida.