Baraza la kijeshi Sudan Lalaani mauaji ya wanafunzi

0
219

Baraza la kijeshi nchini Sudan, limelaani mauaji ya wanafunzi watano waliojumuika na  wenzao katika maandamano ya kulaani  vitendo vya ghasia na vurugu zinaendelea nchini humo.

Akizungumzia hatua hiyo, kiongozi wa Baraza hilo Jenerali Abdel Fattah Al – Burhan amesema mauaji ya wanafunzi hao yaliyotokea hapo jana katika mji wa Eil- Obeid hayakubaliki na  kuongeza kuwa hatua zitachukuliwa kwa watakaobanika kuhusika na mauji ya wanafunzi hao.

Sudan imekuwa ikikabiliwa na maandamano ya mara kwa mara ya kushinikiza utawala wa kiraia tangu jeshi la nchi hiyo lilipomuondoa madarakani aliyekuwa rais wa muda mrefu nchini humo, Omar Al-Bashir, mwezi april mwaka huu.