Kiongozi wa Kanisa Katoliki Dunia Baba Mtakatifu Francis ametoa msaada wa zaidi ya dola laki moja na elfu ishirini za Kimarekani ili kuwasaidia waathirika wa mashambulio yaliyofanywa na wanamgambo katika jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji.
Baba Mtakatifu Francis ametoa msaada wa fedha hizo kufuatia ombi la Askofu wa Kanisa Katoliki katika mji Pemba, -Luis Fernando Lisboa aliyetaka wadau mbalimbali kuwasaidia maelfu ya watu waliyoyakimbia makazi yao kufuatia mashambulio hayo.
Pamoja na mambo mengine, fedha hizo zitatumika kuboresha huduma za afya katika maeneo ambayo watu waliyoyakimbia makazi yao wameweka kambi.
Tangu mwaka 2017 wanamgambo katika jimbo Cabo Delgado lenye utajiri mkubwa wa gesi, wamekuwa wakifanya mashambulio na kusababisha zaidi ya watu Laki nne na elfu thelathini kukosa makazi.