Jeshi la Polisi katika Jimbo la Manica nchini Msumbiji linamshikilia mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 49 kwa kujaribu kuwauza binti zake wawili kwa $120 (TZS 276,036).
Baada ya kukamatwa baba huyo amesema kuwa alitaka kutumia fedha hizo kulipa deni la $65 (TZS 149,519).
Msemaji wa Jeshi la Polisi katika jimbo hilo amesema kuwa mtuhumiwa amekamatwa alipokwenda kuwakabidhi watoto hao wenye miaka sita na nane kwa mnunuzi.
Jeshi la Polisi pia linamshikilia mnunuzi huyo ambaye taarifa zake hazijawekwa wazi.
Polisi wamesema kuwa matukio hayo ya uuzaji wa watoto yanatia hofu ambapo wengi wao hupelekwa kufanyishwa kazi au kwenye ndoa za utotoni.