Baadhi ya miji yaupokea mwaka mpya 2022

0
200

Wananchi katika mji wa Auckland nchini New Zealand wameanza kusheherekea mwaka mpya.

Visiwa vya Tonga, Samoa na Kiribati vilivyopo katika bahari ya Pacific navyo ni miongoni mwa maeneo ambayo yanakuwa ya kwanza kusheherekea mwaka mpya na kufuatiwa na maeneo mengine duniani.

Wananchi katika mataifa mbalimbali duniani wanasheherekea mwaka mpya wa 2022 huku kukiwa na tahadhari kubwa ya kusambaa kwa kasi ya maambukizi ya virusi vya corona.

Mataifa hayo ikiwemo Marekani, Canada, India, Australia na China yanasheherekea mwaka mpya huku Wananchi wake wakiwa katika sheria kali za kuwataka kubakia majumbani na kuepuka misongamano isiyo ya lazima, ili kuzuia maambukizi wakati idadi ya watu wanaopata maambukizi ya corona na kuugua ikiongezeka kwa kasi.

Viongozi mbalimbali duniani akiwemo Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson ametoa salamu za mwaka mpya wa 2022 kwa kuwataka wananchi ambao hawajapata chanjo dhidi ya corona kufanya hivyo, ili kuepuka madhara zaidi kutokana na janga hilo.