Umoja wa Mataifa umemtangaza kiongozi wa kikundi cha wapiganaji wa Moist, Masoud Azhar cha nchini Pakistan kuwa ni moja kati ya watu hatari duniani na amewekwa katika orodha ya magaidi duniani.
Umoja wa Mataifa umefikia hatua hiyo baada ya wapiganaji wa Azhar kuhusika na mashambulio ya kigaidi dhidi ya vikosi vya India, katika jimbo la Kashmir linalodhibitiwa na India.
Mashambulio hayo yalisababisha uhusiano kati ya India na Pakistan kuzorota, huku India ikiishutumu Pakistan kuhusika na mashambulio hayo, jambo lililokanushwa na Taifa hilo.