Awakumbuka wapenzi 42 kwa mkufu wa almasi

0
112

Rapa na mwimbaji maarufu duniani Aubrey Drake Graham anayejulikana sana kama Drake raia wa Canada, ametengeneza mkufu ulionakshiwa madini ya almasi kwa kutumia pete za uchumba ‘engagement rings’ 42 ambazo alipanga kuwavisha wanawake tofauti kwa nyakati tofauti bila mafanikio.

Alex Moss, sonara maarufu wa watu mashuhuri amethibitisha Drake kutengeneza mkufu huo kutokana na pete hizo 42 za uchumba, ikiwa ni idadi ya wanawake ambao aliwaza kuwachumbia na kuwavalisha pete lakini kwa sababu mbalimbali uchumba huo haukuendelea.

“Mkufu huo unaitwa ‘Uchumba Uliopita’, kwa nyakati zote alizofikiria kuchumbia lakini hakufanya hivyo,” ameeleza Moss kupitia video aliyoweka mtandaoni

Takribani miezi 14 imetumika kutengeneza mkufu huo, ambapo kwanza alikuwa na kazi ya kutengeneza pete 42 za wanawake aliowafikiria kuwa wenza wake.

Inaelezwa kuwa Drake amefanya hivyo ikiwa ni moja ya njia ya kuwalumbuka wanawake hao ambao alikuwa na mahusiano nao kwa nyakati tofauti.